Kesi ya Jinai Na. 14691/2026 ilifunguliwa Juni 30, 2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida dhidi ya Washtakiwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Deogratias Gosbert Banuba (aliyekuwa Mganga Mfawidhi), Emmanuel Oswald Matola (Afisa Manunuzi) na Erick Richard Mtega (Mzabuni).
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri na matumizi mabaya ya mamlaka kinyume na vifungu cha 22 na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 (Marejeo ya 2023), kuisababisha mamlaka hasara kinyume na aya ya 10(1) ya Sheria ya Udhibiti wa Makosa ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 Marejeo ya 2019 na utakatishaji fedha kinyume na kifungu cha 12(d) na (e) cha Sheria ya Udhibiti wa Utakatishaji Fedha Sura ya 423 Marejeo ya Mwaka 2019
Inadaiwa kuwa kati ya Disemba 1, 2020 na Julai 30, 20221 mshtakiwa Deogratias Gosbert Banuba aliidhinisha malipo ya Shilingi 73,130,328 kwa Mshtakiwa wa tatu ambaye ni mzabuni. Mshtakiwa namba mbili Emmanuel Oswald Matola na Mshtakiwa wa tatu Erick Richard Mtega walitumia hati ya madai na hati ya mapokezi vifaa kuonesha vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Shilingi 73,130,328 vimepokelewa katika eneo la mradi wakati kiuhalisi vifaa hivyo havikpokelewa.
Mashtaka yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida, Mhe. Allu Nzowa. Mshtakiwa alikana mashtaka yote na amekosa dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Julai 08, 2026 kwa ajili ya hoja za awali.
.png)
0 Comments