UZINDUZI WA WAZO HURU AIR BnB APARTMENTS

 

Mkuu wa wilaya ya Singida Mkoani Singida, Godwin Gondwe amewataka vijana mkoani humo kuwa na macho ya kutazama na kutafsri fursa hususani katika eneo la uwekezaji.

Gondwe ameyasema hayo mkoani Singida katika uzinduzi wa Wazo Huru Air BnB Apartments, zinazomilikiwa na Mwandishi wa habari na mzawa wa Singida Mathias Kanal ambapo amesema Mathias amefanya jambo kubwa na hivyo ndivyo vijana wanapaswa kuwa kwa maana ya kuzitazama fursa kwa ukaribu ,mbali na hapo amempongeza mwekezaji huyo kwa wazo la kujenga nyumba hizo Mkoa wa Singida.

Mmiliki wa Apartments hizo, Mathias Kanal, anasema mradi huo una lengo kubwa la kuchangia eneo la maladhi na kuongeza uchumi wa Mkoa wa Singida huku akisema mradio ho Wazo huru Air BnB Apartments utatatoa huduma nzuri kwa wakazi wa Singida pamoja na wageni kutoka katika maeneo mengine ambao watafika katika nyumba hizo.



Comments