Jamii katika Manispaa ya Singida Mkoani Singida imetakiwa kujenga utamaduni wa kukemea kwa uwazi vitendo vya ukatili, ili kukomesha na kutokomeza vitendo hivyo vinavyoathiri ustawi wa haki za binadamu.
Wito huo, umetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joanfaith Kataraia wakati akifungua kikao cha Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kwa robo ya pili, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Manispaa ya Singida.
Amesema, ukimya wa jamii umekuwa ukichochea kuendelea kwa matukio hayo hivyo ni muhimu kwa wananchi kuweka wazi vitendo vya ukatili na kuvipinga hadharani ili kujenga jamii salama inayozingatia haki na usawa kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shirika la Empower Society Transform Lives (ESTL), Joshua Ntandu amesema, mapambano dhidi ya ukatili yanapaswa kuanzia ngazi ya familia kupitia malezi bora huku akisisitiza kuwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ni muhimu katika kuhakikisha vitendo vya ukatili vinatokomezwa na jamii inakuwa salama kwa kila mwananchi.
Comments
Post a Comment