Leo tarehe 07 Machi 2026, kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida, Bw. Iddi Omari, akimwakilisha Meneja wa Mkoa, kwa kushirikiana na Meneja wa TRA Wilaya ya Manyoni, Bi. Kissame Mathias, wameongoza zoezi la kugawa mahitaji mbalimbali kwa akina mama waliojifungua na wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.
Zoezi hilo lilishirikisha watumishi wote wanawake wa TRA Mkoa wa Singida, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono na kusherehekea mchango wa wanawake katika jamii pamoja na kutoa faraja kwa akina mama walioko hospitalini.


.jpeg)
.jpeg)
0 Comments