TAKUKURU MKOA SINGIDA YASAIDIA KUREJESHA SH MILIONI 119 NA MAGARI MA NNE


Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Singida imesaidia kurejesha kiasi cha Shilingi 119,164,274.88 pamoja na magari manne mali ya taasisi ya SEMA, ambayo yalikuwa yameuzwa kinyume cha Sheria.

Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Petro Horombe ametoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa habari Mjini Singida, ikiwa sehemu ya taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo katika kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025 - 2026.

Ameyataja magari hayo ambayo yamerejeshwa kwa taasisi ya SEMA, kuwa ni pamoja na gari aina ya Isuzu Tipa lenye namba za usajili T423 AED, gari la pili ni Land-rover wanten lenye namba za usajili T412 AED, gari la tau amelitaja kuwa ni Isuzu Tipa linalotumika kubeba vitu vizito lenye namba za usajili  T418 AED na gari la nne lililorejeshwa likiwa ni Toyota VX lenye namba za usajili T465 AED

Horombe amebainisha kuwa Takukuru Singida, imesaidia kurejesha Nyumba kwa Mwananchi mmoja wa Mkoa wa Singida kutoka kwa moja ya Makampuni yanayofanya kazi zake ndani ya mko huo ,ambayo ni dalali wa mahakama ambae alikuwa amejitwalia nyumba hiyo na kuitumia lakini hata hivyo kutokana na kazi ya Takukuru Mkoa wa Singida Mwananchi huyo ameweza kurejeshewa Nyumba yake.

Aidha katika kipindi cha Januari hadi machi 2026, Takukuru Mkoa wa Singida imesema kwa kushirikiana na wadau wengine wa kupinga rushwa wamejipanga kuendelea kufuatilia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika mkoa wa huo, kushirikiana na makundi mbalimbali ya wadau hususani vijana na wanawake katika kutoa elimu inayotoa hamasa kuhusu kupinga na Kupambana dhidi ya janga la Rushwa.

Comments